Moja wapo ni ya vilima hivi ni Pugu Hills.
Milima ya Pugu ni sehemu ya misitu ya hifadhi ya Pugu katika mkoa wa Pwani, Tanzania. Hapa ni karibu na hifadhi ya Misitu ya Kazimzumbwi yote ikiwa imepakana na Selous Game Reserve.
Misitu ya Pugu inasemekana kwamba ni kati ya misitu iliyo na umri mkubwa duniani. Misitu hii ni chanzi cha maji ya mti msimbazi unaopita mpaka maeneo ya Jangwani kuja mpaka Daraja la Salender na kasha kuingia bahari ya hindi.
Katika msitu huu kuna machimbo ya Kaolinite ambayo yaligunduliwa na Mkoloni wa Kijerumani. Ujerumani wamekuwa wakichimba madini hayo kwa muda mrefu tangu walipo tawala Tanzania, ukifika hiko utakuta reli iliyo jengwa kuingia katika machimbo hayo.
Inasemekana kwamba msitu wote upo juu ya madini hayo.
Misitu ya Pugu (Picha kutoka Wikipedia)
Moja ya Lodge zilizopo ndani ya Hifadhi ya Misitu ya Pugu
Moja ya machimbo ya Kaolinite ndani ya Hifadhi ya Pugu
Reli iliyojengwa na Wajerumani kuelekea kwenye machimbo ya Kaolinite
Mawe ya yenye Kaolinite, madini haya yanajulikana kama Kaolin au China Clay (Chanzo: Wikipedia)
Muundo wa kikemikali wa madini ya Kaolinite (Chanzo: Wikipedia)
No comments:
Post a Comment