Thursday 30 June 2016

Hifadhi ya kisiwa cha Rubondo


Hifadhi ya Rubondo ni kisiwa kilichopo pembezoni mwa Ziwa Victoria, ziwa ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani, likiwa linazungukwa na nch tatu, Tanzania, Kenya na Uganda. kimeundwa namkusanyiko wa visiwa tisa vidogo vidogo.

Kisiwa cha Rubondo ni makazi na mazingira muafaka ya kuzaliana samaki wakiwemo sato na sangara. Sangara huweza kuwa na ukubwa wa hadi kilo 100.

Fukwe za kisiwa hiki ni miongoni mwa makazi ya pongo na nzohe. Aidha hifadhi hii ni maskani makuu ya ndege na samaki kama zumbuli, chechele na taisamaki.

Mbali na ndege hao kisiwa hiki ni makazi ya aina nyingine nyingi ya ndege wa majini na mimea kadhaa ambayo hutoa harufu nzuri ya kuvutia.

Wanyama wakazi wa hifadhi hii ni kama viboko, pongo, nzohe, fisi maji, mamba na pimbi wanashirikiana makazi na wanyama waliohamishiwa katika hifadhi hii kama sokwe, tembo, mbega weusi na weupe na twiga.

Namna ya kufika

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 457 na iko kaskazini magharibi mwa Tanzania.Pia hifadhi hii -Inafikika kwa ndege za kukodi kutoka Arusha, Ziwa manyara, Serengeti na Mwanza. -Kwa njia ya barabara kutoka Mwanza -Sengerema-Geita-Nkome kisha kwa boti hadi hifadhini. -Kwa meli ndogo kutoka Muleba na Bukoba vilevile kwa njia ya barabara kutoka wilaya ya Biharamulo na Mulebakupitia kijiji cha Mganza

Chanzo: Wikipedia










 

No comments: