Tanzania imepokea ndege mpya ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) katika hatua ambayo inatarajiwa kuimarisha safari za ndani ya nchi za shirika hilo.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) kutoka Canada ilikotengenezewa.Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamriho aliambia wanahabari kwamba ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja.
Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76 imeingia Tanzania tarehe 20 mwezi wa tisa, ndege zingine tatu zinafuata.
Rais Magufuli alikuwa ameahidi kwamba shirika hilo lingeimarishwa na ndege mpya kununuliwa na sasa YAMETIMIA
No comments:
Post a Comment