Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kutokana na mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na inapatikana katika nchi ya Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theluji.
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia.
- Safari ya kupanda mlima huu humpitisha mpandaji katika kanda za hali ya hewa tofauti kuanzia ile ya nchi za tropiti hadi arktiki.
Kuna njia sita ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi kileleni.
- Njia iliyo rahisi na maarufu zaidi ni ile ya kuanzia lango la Marangu, ambako ndiyo makao makuu ya hifadhi.
Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi
Kuanzia mwezi Desemba hadi februari, na pia mwezi Julai na Septemba (ingawa wakati huu ni baridi zaidi).Chanzo: https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi_ya_Mlima_Kilimanjaro