GEREZA la Kilimo la Songwe lililoko mjini Mbeya, litahamishwa eneo lililopo sasa hivi ili kupisha uchimbaji wa madini ya aina ya Niobium yaliyopo chini ya gereza hilo. Taarifa hiyo imetolewa na mwakilishi wa kampuni ya Panda Hill yenye dhamana ya kuchimba madini hayo.

Kampuni shiriki inayo julikana kwa jina la Panda Hill, imesema wao pamoja na serikali wanapanga kuliamisha gereza hilo. Shughuli ambayo itagharimu kiasi cha shilling za kitanzania Bilioni 400 hii inajumuisha uamishwaji wa nyumba za wafanyakazi pia..


Katika uchimbaji huo wa madini takribani watanzania 467 wanatarajiwa kuajiriwa mara tu zoezi la uchimbaji utakapoanza hapo mwakani. Uchimbaji wa madini hayo unatarajiwa kudumu kwa muda wa maika 30.
Aidha, imeelezwa kuwa eneo hilo ni la nne kugunduliwa kwa madini hayo duniani huku likiwa ni eneo pekee lenye madini hayo barani Afrika. Wakizungumza viongozi wa mkoa wa Mbeya walisema kuwa serikali inatarajiwa kunufaika kupitia jaira, kodi, alisema Mkuu wa Mkoa Amos Makalla.
Chanzo: Swahili times.com


MATUMIZI:

Madini haya yana matumizi makubwa yakiwemo:

- Inachanganywa na chuma na kutengeneza vifaa vigumu kama vile: Injini za Roketi pamoja na Ndege, Mabomba makubwa ya kuptisha vitu vya hatari kama mafuta, kutengenezea vifaa visivyo shika joto

MFANO WA BIDHAA zitokekanazo na Madini ya NIOBIUM:

Engine ya Ndege

Mabomba ya kupitisha vimiminika hatari

Muundo wa NIOBIUM

Injini ya Kifaa cha kwenda anga la juu sana (kama Mwezini n.k)



Kifaa cha Mionzi(MRI) kifaa hiki pia kinatumia GESI ile iliyo gundulika hivi karibuni (Gesi ya HELIUM).


HISTORIA:

Madini haya yanatumiwa sana na nchi zilizoendelea kiteknolojia.

Duniani huu ni Mgodi wa Nne Pekee kugundulika duniani.